Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyamapori waua watu 15 Kanda ya Ziwa

Wanyamapori Picbnhjn Wanyamapori waua watu 15 Kanda ya Ziwa

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Jumla ya watu 15 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa na wanyama wakali katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2022 baada ya wanyama hao kuvamia makazi ya watu.

Watu hao wamefariki kufuatia kuwepo kwa matukio 391 yaliyoyokea katika vijiji vinavyozunguka mapori manne ya akiba yaliyopo kanda ya ziwa baada ya wanayama hao wakali kuvamia makazi ya watu pamoja na mashamba.

Akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Mara aliyefanya ziara ya kukagua shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) wilayani Serengeti leo Alhamisi Februari 23, 2023, Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Ziwa, Said Kabanda amesema kuwa katika kipindi hicho walifanya doria 339 kuhakikisha usalama wa wakazi hao.

"Wanyamapori ambao wamekuwa na tabia ya kuvamia na kufanya uharibifu ni pamoja na tembo, simba, fisi, viboko, mamba, nyati na chui na sisi pamoja na mambo mengine tuna wajibu wa kdhibiti matukio hayo kwa usalama wa watu na mali zao na mapori ya akiba ya kanda ya ziwa ni pamoja na Ikorongo, Grumeti, Kijereshi na Maswa,” amesema.

Amefafanua kuwa wanyamapori hao wamekuwa na tabia ya kuvamia mashamba na wengine kufika hadi kwenye makazi ya watu na kula chakula lilichovunwa na kuhifadhiwa sehemu mbalimbali ikiwepo kwemye maghala.

Amesema kuwa katika matukio hayo wilaya zilizoathirika zaidi ni pamoja na Bunda, Musoma na Serengeti mkoani Mara na Itilima, Bariadi na Busega mkoani Simiyu na kuongeza kuwa kuanzia mwaka mwaka 2016 hadi 2021 Serikali ililipa zaidi ya Sh2.3 bilioni kama kifuta machozi kwa wahanga 13,540 wa matukio hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee pamoja na mambo mengine ameiagiza Tawa kuanzisha bucha ya nyamapori wilayani Serengeti ambayo itatumika kama sehemu ya mafunzo kwa watu wenye nia ya kuanzisha mabucha hayo.

"Mambo mengine huwa mnayasababisha nyie, hivi kweli hifadhi ya Serengeti ipo mkoani Mara halafu kuna bucha moja tu mengine yapo Mwanza halafu mnasema moja ya changamoto hapa ni uwindaji wa nyama (vimoro)?

Kwa nini msifungue bucha ya mfano ili watu wajifunze na kujua taratibu na hatimaye wafungue bucha hizo kwa wingi ili watu wapate nyama kwa urahisi na halali," amesema

Mkuu huyo wa mkoa pia amewataka viongozi kuwahimiza watu wao kuachana na vitendo vya ujangili ili mamlaka zinazohusiana na uhifadhi kuhangaika na masuala ya unahili na badala yake wajihusishe zaidi na masuala ya uwekezaji.

Chanzo: mwanachidigital