Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanunuzi wa dada poa kusakwa

Dada Poapoa Wanunuzi wa dada poa kusakwa

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wa Shinyanga Christina Mndeme ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya doria za mara kwa mara ili kuwakamata wanawake wanaofanya biashara ya ngono pamoja na wateja wao kwani serikali hairuhusu biashara hiyo haramu.

"Kamateni anayefanya biashara, mteja wake, mlinzi wake pamoja mmiliki wa nyumba inayohifadhi wanafanyabiashara ya ngono, tunataka kila mmoja afanye kazi halali, wengine wanajificha kwenye biashara hii na kufanya uhalifu ikiwemo wizi, bidhaa na mnunuzi wa biashara hiyo wote kamateniā€ amesema Mhe. Mndeme.

Mndeme ametoa maagizo hayo wakati akiendelea na ziara yake kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live