Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanufaika waishukuru TASAF wilani Magu

7ab225d6bcf3b4f73c558159aefafd14 Wanufaika waishukuru TASAF wilani Magu

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WANUFAIKA wa kaya maskini zilizo katika mpango wa mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) wilaya Magu wameupongeza mfuko huo kwa kuweza kuwaboresha maisha yao.

Akizungumza na gazeti hili,Mkazi wa kijiji cha Ndagalu, Suzana Nzwekemla amesema anaushukuru mfuko huo umemsaidia aliweza kununua mifugo ya kondo 20 na kuanza kujihusisha katika ufugaji.

Alisema kupitia ruzuku hizo anawasomesha wajukuu zake wawili katika shule ya msingi Ndagalu. Alisema pia amefanikiwa kujenga nyumba moja.

Alisema kupitia pesa hiyo amefanikiwa kujihusisha katika kilimo cha zao la Choroko pamoja na Mahindi.

Mwenyekiti wa kikundi cha kikundi cha Nyakarungu A- Tasaf ,Martha Mashauri alisema kupitia ruzuku ya mfuko huo wamefanikiwa kununua mashine ya kuvutia maji kwenye mashamba wakati wa kilimo.

Alisema kupitia mashine hiyo wamefanikiwa kupata fedha ya kuweza kukodisha mashamba kwajili ya kulima mazao ya Mahindi na Mpunga.

Mashauri alisema kupitia Tasaf,Halmashauri ya Magu imeweza kuwaamini na kuwakopesha kiasi cha fedha shilingi milioni 2/- ambayo wamekuwa wakirejesha kidogo kidogo.

Alisema anaiomba Serikali iendelee kuwasaidia wananchi wake.

Afisa ufuatiliaji wa TASAF,wilaya ya Magu Lina Marealle alisema kwa wilaya yake kuna kaya 5488 za wanufaika katika vijiji 62.

Marealle alisema lengo la TASAF ni kuziwezesha Kaya maskini kwa kuongeza kipato, fursa na kuongeza ufanisi katika matumizi ya chakula, afya na elimu.

Alisema wamekuwa wakitoa ruzuku na asilimia kubwa wanufaika wengi wamekuwa wakijikomboa kimaisha kwa kujiajiri katika kilimo na ufugaji.

Chanzo: habarileo.co.tz