Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne waponzwa na vichwa vya fisi

WATU 2AA Wanne waponzwa na vichwa vya fisi

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majangili wamekamatwa na jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu, katika vijiji vya Muungano na Lusahunga wilayani Biharamulo mkoani Kagera, wakiwa na nyara za serikali ambazo ni meno mawili ya tembo, ngozi ya fisi, kichwa cha fisi, vipande vitatu vya ngozi ya nyati, mkia wa nyati, ngozi ya swala na silaha mbili aina ya gobore zikiwa na risasi tatu za gololi ambazo hutumika kuua wanyamapori.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa hifadhi ya Taifa ya Ibanda - Kyerwa, ACC. Fredrick Mofulu amesema kuwa watu hao walikamatwa na askari wa Hifadhi za Taifa za Ibanda ya wilayani Kyerwa na Rumanyika ya wilayani Karagwe Februari 13 mwaka huu, baada ya kupata taarifa za kiintelijensia za uwepo wa mtandao wa watu wanaojihusisha na ujangili wa wanyama pori pamoja biashara ya nyara za serikali.

Mofulu amewataja waliokamatwa kuwa ni Raphael Lugaira (44), Fikiri Lugaira (43), Majaliwa Charles (42) na Warwa Rupilya (45) wote wakazi wa Wilaya ya Biharamulo.

"Baada ya watuhumiwa hao wa ujangili kukamatwa na kikosi cha askari wa jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu lililopo chini ya TANAPA tulishirikiana na jeshi la polisi wilaya ya Biharamulo, katika hatua mbambali ikiwemo kazi za upelelezi na ufunguaji wa majalada ya kesi" amesema Mofulu.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera William Mwampaghale amesema kuwa wamekuwa wakifanya oparesheni katika Hifadhi zote ikiwamo za Ibanda - Kyerwa, Rumanyika -Karagwe na Burigi - Chato kwa kwa kushirikiana na watu wa Hifadhi, lengo likiwa ni kuhakikisha vitendo vya ujangili vinakomeshwa, na kwamba watu hao watafikishwa katika vyombo vya sheria.

"Nitoe wito kwa wananchi wa Kagera, kutoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwamo ujangili, maana watu hawa tunaishi nao katika jamii" amesema Mwampaghale.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live