Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wafariki, tisa wajeruhiwa Geita

Mklll Wanne wafariki, tisa wajeruhiwa Geita

Wed, 1 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika matukio matatu tofauti yakiwemo mawili ya ajali za barabarani na mvua ya mawe iliyoambatana na upepo iliyoezua na kubomoa nyumba za wananchi wa Kata ya Bukoli Wilaya ya Geita.

Katika tukio hilo la mvua, mtoto Merisiana Lucas (5) amepoteza maisha huku watoto wengine, Silvester Juma (10) na Abdala juma (2) wamejeruhiwa.

Akito taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Geita, Cornel Magembe jana Jumanne Februari 28, 2023, Ofisa Mtendaji Kata ya Bukoli, Nasoro Mgasa amesema zaidi ya watu 1, 000 wameathirika na mvua hizo zilizozikosesha makazi kaya 13 kati ya kaya 117 zilizoathirika.

“Baadhi ya kaya zimekosa chakula kutokana na akiba yote waliohifadhi kuharibiwa na mvua hizo,” amesema Ofisa Mtendaji huyo huku akitaja kijiji cha Bugogo kuwa ndicho wakazi wake wameathiriwa zaidi.

Mkuu wa Wilaya amewapa pole wananchi waliothirwa na mvua hizo huku akiwaagiza wataalam wa Halmashauri ya Geita kufanya tathmini ya haraka kujua ukubwa wa madhara yaliyotokea na msaada wa haraka unaohitajika kwa wananchi zaidi ya 1, 000 walioathirika.

Katika tukio nyingine, watu watatu wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa katika ajali mbili za gari zilizotokea katika maeneo mawili tofauti mjini Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema ajali ya kwanza ilitokea eneo la Mtakuja barabara ya kwenda Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) baada ya gari aina ya Subaru Forester iliyokuwa inaendeshwa na Aron Mashosho (30) kumgonga mwendesha baiskeli ambaye hajafahamika jina na kufariki papo hapo.

Dereva wa gari hilo amejeruhiwa vibaya na amekimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa matibabu zaidi.

Kamanda Jongo amesema katika tukio la pili, dereva wa gari aina ya Toyota Vios, Sospeter Pascal (46) alifariki dunia baada ya gari hilo kupinduka kutokana na kushindwa kulimudu gari hilo alipojaribu kulipita lori la mchanga.

Ndani ya gari hilo walikuwemo watoto sita ambao mmoja wao amejeruhiwa vibaya kichwani huku wengine watano wakipata majeraha madogo madogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live