Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wafariki ajalini mkoani Kigoma

Sun, 1 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kigoma. Watu wanne wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda kupinduka.

Ajali hiyo imetokea jana  Alhamisi Juni 28, 2018  eneo la mlima Kasagamba Wilaya ya Kigoma. Gari hilo lilikuwa likitokea Kalinzi kwenda Kigoma Ujiji.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno ameieleza MCL Digital leo Ijumaa Juni 29, 2018 kuwa katika uchunguzi wa awali wamebaini chanzo cha ajali ni mwendo kasi uliosababisha dereva kushindwa kulimudu gari.

Amewataja waliopoteza maisha kuwa ni Yasinta Yohana (60), Consolata Boniphace (40), Irene Lumambo (55) na Sevelin Robart (60).

"Majeruhi 22 wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Maweni,” amesisitiza.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kigoma ya Maweni,  Osimundi Diegula amesema miili ya marehemu ilifikishwa katika hospitali hiyo jana Juni 28, 2018, “na majeruhi wa ajali hiyo pia walifikishwa hospitali.”

Mmoja wa majeruhi, Theresia Daudi amesema ajali hiyo imetokea wakiwa njiani kuelekea Kigoma mjini, kwamba walikuwa wakitokea katika kijiji cha Kalinzi katika sherehe ya kumpongeza msichana anayetarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Chanzo: mwananchi.co.tz