Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanne wa familia moja wajeruhiwa vibaya na fisi

Fisi Kiganja Fisi

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wa familia moja wakazi wa kijiji cha Kilino kata ya Isanzu Wilayani Nzega Mkoani Tabora wamejeruhiwa vibaya na Fisi maeneo mbalimbali ya miili yao wakati wakiwa shambani wakinyunyuzia dawa katika mimea ya pilipili hoho

Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora ACP. Richard Abwao amesema Fisi huyo ambaye alizuka kutoka mahala pasipo julikana aliwavamia wanafamilia hao waliokuwa wakiendelea na shughuli zao shambani na kuwararua vibaya maeneo mbali mbali ya miili yao hasa katika upande wa mikono yao .

Kamanda amesema wakazi wa eneo hilo wamefanikiwa kumuua Fisi huo, huku hali ya majeruhi ikitajwa kuendelea vizuri baada ya kukimbizwa Hospitali kwa ajili ya matibabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live