Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake watakiwa kuwa wamoja, kushirikiana

Wed, 28 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wanawake walioko katika harakati wa rika zote wametakiwa kuungana na kujenga umoja utakaowawezesha kubeba agenda zao kuzipeleka mbele zaidi na kuzitekeleza.

Wito huo umetolewa leo Jumanne Agosti 27, 2019 na mkurugenzi wa shirika la Msichana Initiative, Rebeka Gyumi katika mkutano wa wawakilishi wa makundi ya wanawake waliko katika harakati.

Pamoja na mambo mengine, shirika hilo  linajishughulisha na haki ya mtoto wa kike katika elimu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo,  Gyumi amesema wanawake hata kama watakuwa na agenda,  kama hawataamua kuwa pamoja ni vigumu kubeba agenda zao.

“Kuna nguvu nyingi zinatugawa kwa maslahi tofauti ya kisiasa na kifedha. Ni  lazima tufanye jitihada za makusudi kuhakikisha wasichana na wanawake tunajenga umoja wetu ili kubeba agenda zetu na kuzipeleka mbele zaidi,” amesema Gyumi.

 

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz