Wed, 12 Dec 2018
Chanzo: mwananchi.co.tz
Rukwa. Wanawake wilayani Nkasi mkoani hapa wametakiwa kuacha utegemezi badala yake, wajishughulishe na uzalishaji ili kujenga heshima ndani ya familia zao. Hayo yalisemwa juzi na mkuu wa wilaya hiyo, Said Mtanda akifunga mafunzo ya kuwajengea uwezo wasichana waliopata mimba utotoni yaliyofanyika Sekondari ya Mkwamba. Naye mratibu wa mradi huo, Nestory Frank alisema wasichana 381 wamenufaika na mafunzo hayo. (Mussa Mwangoka)
Chanzo: mwananchi.co.tz