Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake wajazana Kongamano la 'Wonder Women'

49719 WONDER+PIC

Mon, 1 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza katika kongamano la ‘Wonder Women’ lililoandaliwa na mtangazaji maarufu Tanzania, Zamaradi Mketema.

Kongamano hilo ambalo ni mara yake ya pili kufanyika, linafanyika leo Jumapili Machi 31, 2019 katika Ukumbi wa Kisenga uliopo jengo la Millennium Tower, Makumbusho, Jijini Dar es Salaam.

Mwananchi limeshuhudia wakina mama wakimiminika kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kuhudhuria kongamano hilo ambalo lengo lake hasa ni kuzungumzia masuala yanayohusu wanawake.

Kutokana na mwitikio huo wa wanawake, waandaaji wamelazimika kuongeza viti kwa kuwa vilivyopo maalum kwa ajili ya ukumbi huo vilikuwa vimejaa huku ukumbi huo ukiwa na uwezo wa kuchukua watu 3,000.

Kwa upande wake, Zamaradi amesema amejisikia faraja kwa wanawake hao kujitokeza na kuongeza kuwa imeonyesha namna gani wameanza kujitambua.

Amesema mambo mbalimbali yatajadiliwa kuhusu wanawake ikiwemo kujikinga dhidi ya ugonjwa wa saratani.

Baadhi ya wanawake waliofika akiwemo Teddy Goliama, amesema amevutiwa kwenda kwenye kongamano hilo kutokana na kuwa sehemu inayokutanisha wanawake mbalimbali.

Teddy amesema akiwa kama mjasiriamali wa kupika chakula na biashara ya madini anaamini atapata mtandao mpana wa kufanya nao kazi.

Theresia Raphael, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema kongamano hilo ni moja ya eneo la kupata elimu na kuongeza kuwa elimu si ile ya darasani tu na ndio maana mwitikio wa watu umekuwa mkubwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz