Wed, 3 Nov 2021
Chanzo: eatv.tv
Mama mmoja mkazi wa Arusha, Mianzini kwa Mollel, ameiomba serikali kuingilia kati utata ulioibuka kuhusu mwanaye Happy, baada ya mama mwingine mkazi wa eneo la Unga limited, kujitokeza na shuleni na kumlipia pesa ya chakula akidai Happy ni mtoto wake wa kuzaa na anayeishi naye ni mlezi tu.
EATV imefika katika eneo la Mianzini kwa Mollel na kuzungumza na mama anayeishi na mtoto Happy kwa miaka yote akiwa mama yake mzazi, na kusema anasikitishwa na kitendo cha mwanamke mwenzake kusema uongo na kuzua taharuki kubwa.
Chanzo: eatv.tv