Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake  wa TALGWU wakabidhi misaada kituo cha wahitaji

11ef320e6fe9548a1ea9fe334281780c Wanawake  wa TALGWU wakabidhi misaada kituo cha wahitaji

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA Cha wafanyakazi wa Serikali za mitaa (TALGWU), kupitia Kamati ya Ushauri ya Wanawake ngazi ya taifa na mikoa kimetembelea kituo cha wahitaji cha Masista wa Maria Tereza kilichopo Hombolo na kukabidhi zawadi mbalimbali kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza juzi wakati wa mahojiano kwenye sherehe ya Siku ya Wanawake Duniani, Mwenyekiti wa Taifa wa kamati ya ushauri ya wanawake, Beatrice Njawa alisema waliamua maadhimsho ya mwaka huu kila Kamati ya Wanawake Mkoa kufanya maadhimisho hayo kwa kutanguliwa na kujichangisha na kupeleka mahitaji kwa wahitaji.

"Wanawake tulikubaliana kutoa vitu visivyotumika vyenye ubora kama nguo , viatu kwa kituo hiki ili vitu hivi wavigawe kwa wasiojiweza wanaoishi nje ya kituo,”alisema Njawa.

Kutokana na mlipuko wa corona, alisema Njawa, kamati ilipewa taarifa na uongozi wa kituo kuwa hawataweza kuwaona wahitaji ila sadaka zitapokelewa na wao wakazifikisha.

Kituo hicho kina wahitaji watoto yatima, wazee wasiojiweza na mabinti.

Wanawake wa kamati ya kitaifa waliofika kituoni hapo ni wale wa kutoka mkoa ya Kigoma, Lindi, Mtwara, Mbeya , Dar es Salaam, Geita na Dodoma. Pia viongozi wa TALGWU wanaume wamechangia michango hiyo.

Alisema mbali na nguo na viatu vitu vingine vilivyotolewa ni mchele, unga, sabuni, mafuta na sukari.

Alisema kwamba nia kubwa ya misaada hiyo ni kuchangia juhudi za kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha kuwa wenye mahitaji ili watoto wa kike wawe wanaandaliwa vyema kushiriki katika nafasi za maamuzi na uongozi.

Siku ya Mwanamke Duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walioandamana mjini New York wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura.

Chanzo: www.habarileo.co.tz