Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake hatarini kupata vibiongo

6919d901270ab52aeb92ae6af686dc5f Wanawake hatarini kupata vibiongo

Sat, 26 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANAWAKE wanatajwa kuwa hatarini zaidi mara tano kupata tatizo la kibiongo kuliko wanaume huku vinasaba vikitajwa kuchangia tatizo hilo.

Dakatri Bingwa wa Upasujia wa Ubongo na Mgongo, Juma Mzimbiri kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili(MOI) ameiambia HabariLeo kuwa mama mwenye kibiongo anauwezo wa kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo kwa asilimia 50.

Dk Mzimbiri ametaka watoto kuanzia miaka mitano wachunguzwe afya zao ili atakayebainika aweze kupata matibabu ya tatizo hilo kwa haraka.

“Hakuna sababu za moja kwa moja kisayansi zinazohusishwa pia kuna tatizo la umri na tatizo hilo hivyo watu wajue kuwa matibabu yapo na tatizo linatibika nawashauri wawahi hospitali lakini sula la kufanya uchunguzi kwa watoto hasa wa shule ni muhimu,”anabainisha .

Dk Mzimbiri amesema unyanyapaa katika jamii unawaathiri kisaikolojia watu wenye tatizo la kibiongo.

“Baadhi wa wenye tatizo wanazaliwa nayo lakini wengine wanapata tu hakuna uhusiano na ubebaji mzigo au begi za shule na tatizo hili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz