Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaume 2008 waliotelekeza watoto watii amri ya RC Makonda

7172 WhatsApp Image 2018 04 27 At 18.01.57.jpeg TZW

Sun, 29 Apr 2018 Chanzo: bongo5.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Ijumaa hii amefunga zoezi la kutafutia haki watoto waliotelekezwa kwa mafanikio makubwa ambapo zaidi ya Kinababa 2,008 wamekubali kwa maandishi kutoa Pesa ya Matunzo ya Mtoto huku Watoto 2,971 wakiandikishwa kwaajili ya kupatiwa Bima ya Afya Bure.



Akitoa tathimini ya zoezi hilo lililohitimishwa leo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo zaidi ya Wananchi 17,000 walijitokeza kwaajili ya kupata huduma na Kati ya hao wananchi 7,184 wamesikilizwa huku wananchi 10,000 wakiwa bado hawajasikilizwa na Wananchi 270 wakipimwa DNA.

Kutokana na ukubwa wa tatizo la familia kutotekeleza vyema majukumu yake RC Makonda ameunda Kamati ya Wataalamu 15 wakiwemo Wanasheria, Maafisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na Asasi za kiraia itakayofanya kazi ya kupitia mapungufu ya kisheria na Changamoto zilizojitokeza kisha kutoa mapendekezo kwaajili ya kufikishwa kwa mamlaka husika kwaajili ya maboresho ambapo kamati hiyo itaanza kazi May 05 chini ya Mwenyekiti wake Wakili Albert Msando.

Aidha RC Makonda amesema tayari amekabidhi Jeshi la Polisi majina ya kinababa waliokaidi wito wake ambapo kwa wale walioko Mikoani barua zitapelekwa kwa Wakuu wa Mikoa na waliopo Nje ya Nchi majina yatafikishwa kwenye Ofisi za Ubalozi kwaajili ya utekelezaji.

Hata hivyo RC Makonda amesema kupitia zoezi hilo limefanikisha watoto wawili wenye asili ya China kupata matunzo hadi watakapokuwa wakubwa chini ya jumuiya ya Watu wa China.

Pamoja na hayo RC Makonda amewashukuru wanasheria, maafisa ustawi wa jamii, dawati la jinsia, wataalamu kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali na vyombo vya habari kwa kushirikiana nae bega kwa bega kufanikisha Zoezi hilo.

Chanzo: bongo5.com