Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaouza kadi za kliniki kuchukuliwa hatua

GWAJIMA WEB Dorothy Gwajima, Waziri wa Afya

Tue, 16 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Dkt Dorothy Gwajima amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote Nchini kufuatilia mienendo ya watumishi wa Afya katika Hospitali Vituo vya Afya na Zahanati wanaokiuka sheria za nchi na utaratibu wa utumishi wa umma.

Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa na tabia ya kuwatoza wakina mama wajawazito kwa kuwauzia kadi za Kliniki kati ya shilingi 2000 hadi shilingi 5000 ili watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.

Amebainisha hayo wakati akizindua mpango maalumu wa utekelezaji wa watoto wachanga Nest 360 katika hospital ya Rufaa Mkoa wa Temeke Jijini Dar es salaam ambayo imeboresha huduma kwa kihudumia watoto kutoka watoto 20 Mwaka 2019 hadi kufikia watoto 70 mwaka 2021 kwa siku hali iliyopunguza msongamano katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live