Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaotumia jina la RC Sanare kukiona

92527 Pic+sanare Wanaotumia jina la RC Sanare kukiona

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewatahadharisha wakulima na wafugaji kuacha kutumia jina lake vibaya ili kufanya uhalifu.

Mkuu huyo alisema hayo juzi alipokutana na wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Kilosa wakiwamo wanaotuhumiwa kuwa chanzo cha migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

Sanare alisema tangu kufika mkoani hapa, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakilisha au kupitisha mifugo yao katika mashamba ya wakulima na kudai kuwa hawawezi kufanywa lolote kwa kuwa mkuu wa mkoa aliyepo ni kabila moja.

Aliwataka wafugaji kuacha mara moja kutumia jina lake kwa kisingizio cha ukabila kwa kuwa hakuletwa mkoani hapa kwa ajili ya wafugaji pekee bali wananchi wote.

Mkulima Kulwa Dongo wakulima alisema kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya kushamiri kwa mifugo inayokula mazao yao.

Mfugaji Amini Kaundula akadai kubambikiwa kesi za kulisha mifugo mashambani na kwamba yeye hafanyi hivyo na amekuwa akilisha kwenye maeneo waliopangiwa.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz