Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaopata virusi Omicron 70% hawahitaji hospitali

7c94e5fc22071d45eb4a8afe1aadbc37.jpeg Kirusi Kipya cha Omicron kimesambaa katika nchi mbali mbali Barani Afrika

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Watafiti wanaoangalia maambukizi ya virusi vya corona wamesema watu wanaopata kirusi cha Omicron wana uwezekano mdogo wa kuhitaji huduma ya hospitali.

Watafiti hao wamesema kwamba asilimia 50 hadi 70 ya wanaopata kirusi hicho kipya huenda wasihitaji huduma za hospitali kama mawimbi mengine ya awali ya virusi vya corona.

Wakala wa Usalama wa Afya wa Uingereza walioendesha utafiti huo, wamesema hata hivyo pamoja na ukweli huo kirusi hicho kipya kinaweza kuwapeleka watu wengi hospitalini.

Taarifa kutoka Wizara ya Afya nchini Uingereza imesema kutokana na mazingira ya sasa ya kirusi hicho, ni mapema sana kuamua hatua zijazo za kukabiliana nacho.

Aidha, imesema uwezo wa chanjo ya corona kukabiliana na kirusi hicho kipya inapotea wiki 10 baada ya mtu kupata chanjo ya pili ya uimarishaji.

Imeelezwa kuwa, pamoja na ukweli huo, kirusi hicho kinaweza kusababisha kuelemewa kwa hospitali kutokana na kasi yake ya maambukizi. Haijajulikana kwa kina nini kitatokea kama watu walio na umri mkubwa wakipata maambukizi hayo.

Uingereza imesema watu wengi walioonekana na kirusi hicho kipya walikuwa na umri chini ya miaka 40.

Wakala ya Usalama wa Afya nchini Uingereza (UKHSA), Dk Jenny Harries alisema utafiti wao umeonesha wanaokumbwa na kirusi hicho wengi wao hawana sababu ya kukimbilia hospitali kuliko wanaoambukizwa virusi vingine vya awali.

Pia imeelezwa kuwa, uwezo wa chanjo kuwakinga waliochanjwa dhidi ya Omicron ulikuwa chini, ingawa walipaswa kuchoma chanjo kwa mara ya pili ya uimarishaji.

Ofisa Mtendaji wa Hata hivyo, amesema uwezo wa kukinga ulipungua kwa asilimia 15 na 25 baada ya majuma 10.

Chanzo: www.habarileo.co.tz