Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaopandisha nauli za daladala Dar kukiona

Daladala Nauli Kupanda Wanaopandisha nauli za daladala Dar kukiona

Wed, 4 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imewaonya madereva wa daladala wanaopandisha nauli bila kufuata utaratibu na kueleza kuwa endapo watabainika wachukuliwa hatua.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 4, 2023 na Ofisa Mfawidhi wa Latra Kanda ya Dar es Salaam.

Katika kero hiyo Hanifa Masanja, Mkazi wa Kiwalani alihoji Latra, kama “kweli inajua majukumu yake? Na kwa nini mabasi ya abiria maarufu daladala jijini Dar es Salaam, yanawatoza abiria nauli maradufu?”

Amesema: “Utaona ukifika muda wa usiku, kama sehemu nauli ni Sh500 basi wao wanatoza Sh1,000.”

Abiria wa njia kama Buguruni, Ubungo kwenda Gongo la Mboto, Mbagala ni waathirika sana. Najua hata njia nyingine za jiji hilo, tatizo ni hilohilo

Kwa nini Latra haiweki watu wa kuwachukulia hatua wenye mabasi, kwa sababu wakifanya hivyo mara kwa mara, hawa wataacha tu. Latra kwani inafanya kazi gani?

Acheni kujifungia ofisini, nendeni kufanya doria katika vituo ili msaidie wakazi wanaoumia.

Kondo amesema Latra haitawavumilia madereva wanaoongeza nauli za mabasi bila kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka hiyo.

“Mara nyingi waendeshaji wa mabasi huongeza nauli nyakati za usiku hili lazima likomeshwe ili kuepusha usumbufu usio wa lazima kwa wasafiri, au kufungiwa leseni ya utoaji huduma kwani ni kinyume cha sheria kupandisha nauli bila kibali cha mamlaka,”alisema Kondo.

Kondo amesema mamlaka hiyo imekuwa ikipeleka maafisa wake katika njia zinazobainika kuwa na tabia hiyo ili kuwapa uelewa abiria na madereva juu ya kitendo hicho

“Latra itamchukulia hatua dereva yeyote atakayebainika kupandisha nauli kinyume na utaratibu, atakayebainika atalipa faini ya Sh250, 000 au kufutiwa leseni yake. Abiria wasikubali kulipa fedha zaidi, anapaswa alipe nauli iliyowekwa na Latra,” alisema.

Amebainisha kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo Latra imetoa namba ambazo zimebandikwa kwenye baadhi ya mabasi na kwenye vituo.

"Ikiwa abiria atatozwa nauli kubwa tofauti na iliyopangwa na mamlaka, anapaswa kupiga namba hiyo ambayo ni bure,”.

Chanzo: mwanachidigital