Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanaodaiwa kuuawa na wafugaji Kigoma watambuliwa

Kigoma Rpc Pic Wanaodaiwa kuuawa na wafugaji Kigoma watambuliwa

Fri, 3 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu waliofariki dunia katika mapambano kati ya maofisa misitu na wafugaji waliovamia Hifadhi ya Kijiji cha Chakulu Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wametambulika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Filemon Makungu amewataja waliofariki katika tukio hilo lililotokea juzi Jumatatu Januari 31, 2023 kuwa ni Adam Alenga ambaye ni Afisa Misitu Wilaya ya Uvinza na askari wawili wa jeshi la akiba (mgambo) ambao ni Ibrahim Seba (37) na Moshi Shaban (35).

Askari mgambo wanne walijeruhiwa katika tukio hilo huko wenzao watano watano, kati yao, watatu wakiwa na silaha waliripotiwa kutojulikana walipo.

Akizungumzia tukio hilo leo Alhamisi Februari 2, 2023, Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani emeviagiza vyombo vya dola kuendelea na msako dhidi ya wote waliohusika katika tukio hilo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

“Wasakwe popote walipo hadi wapatikane; hata kama wako porini wasakwe huko huko,” ameagiza Mkuu huyo wa wilaya aliyeapishwa kushika nafasi hiyo wiki hii.

Tukio lilivyokuwa Maofisa misitu pamoja na mgambo waliohusika katika tukio hilo walikuwa katika doria ya kawaida ndipo walipokamata mifugo iliyokutwa ikichungwa ndani ya eneo la hifadhi ya Kijiji cha Chakulu kwa hatua zaidi za kisheria.

Baada yay a mifugo yao kukamatwa, wafugaji wanadaiwa kupiga yowe iliyowakusanya wananchi walioanza kuwaandamana maofisi misitu na askari mgambo waliokuwa wanatekeleza wajibu wao wa kulinda hifadhi.

Kutokana na kundi kubwa la wananchi waliojihami kwa silaha za jadi kuonyesha nia ya kukabiliana nao, maofisa misitu na mgambo waliamua kuachia mifugo yote waliyoikamata na kuelekea eneo walikoegesha magari yao kwa lengo la kujinusuru lakini huko nako wakakuta kundi kubwa zaidi la wananchi amba walioanza kuwashambulia kwa mawe na silaha za jadi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live