Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa wanusurika kufa kwa kuangukiwa na ukuta

Ukuta Chatooo.png Ukuta

Fri, 29 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wawili ambao ni wanandoa, Wiliamu John (65) na mkewe Melesiana Hamidu (63) wakazi wa Kijiji cha Kijuka Kata Nyamazugo Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamenusurika kifo baada ya kudondokewa na ukuta wa nyumba yao alfajiri ya juzi wakiwa wamelala.

Baada ya tukio hilo wanandoa hao walimbikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya matibabu ambapo wamelazwa katika chumba cha dharula huku Afisa tabibu wa zamu kitengo cha dharula Hospitali hapo Dk Kephlen Kaswahili amesema hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.

"Tumewapokea asubuhii ya leo hali zao hazikuwa nzuri tunaendelea kuwapatia matibabu na hali zao zinaendelea vizuri Wiliamu John anamaumivu kwenye kifua na nyonga, Melesiana Hamuduni yeye anamaumivu kifua na miguu' amesema Dkt Kaswahili.

Diwani wa kata ya Nyamazugo, Enock Sengerema amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika kata hiyo zimeendelea kuleta madhara ikiwo nyumba zisizo imara kudondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live