Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa waliotengana wapatanishwa na polisi

Wanadoa Patano (600 X 440) Wanandoa waliotengana wapatanishwa na polisi

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea siku ya Wapendanao Duniani ambayo huadhimishwa Februari 14 ya kila mwaka, Jeshi la Polisi mkoani Iringa limefanikiwa kuwapatanisha Wanandoa Dotto Mgongolwa na Sina Mwengele katika kituo cha Polisi cha Kalenga.

Mapatanisho hayo yamesimamiwa na Mkuu wa kituo cha Polisi cha Kalenga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Samwel Kafula alipokuwa akitoa elimu juu ya madhara ya unyanyasaji wa kijinsia kwa Wanandoa hao waliofika kituoni hapo.

Kutokana na mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia, Wanandoa hao Dotto na Sina walifikia hatua ya kutengana na kugawana vyombo.

Wanandoa hao wanadaiwa kupigana mara kwa mara na kushtakiana hadi Polisi kuingilia kati, na baada ya kusuluhishwa wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuwapatanisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live