Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa waangukiwa na ukuta wakiwa wamelala

Wanandoa Ukuta.png Wanandoa waangukiwa na ukuta wakiwa wamelala

Wed, 27 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanandoa wawili mkoani Mwanza wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba walipokuwa wamelala.

Wanandoa hao, Wiliamu John (65) na mkewe Melesiana Hamidu (63) ambao ni wakazi wa Kijiji cha Kijuka Kata Nyamazugo wilayani Sengereme Mkoa wa Mwanza wamekutwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo Jumatano Desemba 27, 2023.

Kutokana na majeraha waliyopata, wanandoa hao walikimbizwa katika hospitali teule ya wilaya hiyo katika chumba cha dharura wanakopatiwa matibabu.

"Tumewapokea asubuhii ya leo na hali zao hazikuwa nzuri, tunaendelea kuwapatia matibabu na hali zao zinaendelea vizuri,” amesema Ofisa tabibu wa zamu katika hospitali hiyo, Dk Kephlen Kaswahili.

Akieleza tukio hilo hospitalini hapo, Melesiana ameelaza kuwa saa 5:30 alitoka nje kwenda hajandogo huku mvua ikiwa inanyesha alimwacha mume akiwa amelala na baada ya kurejea ndani, alisikia kama kishindo nje lakini aliendelea kulala.

Alisema baada ya dakika kadhaa wakiwa wamelala na mumewe wakaangukiwa na ukuta uliowafunika.

Naye John amewashukuru wananchi waliofika kuwasaidia maana walikuwa wamepoteza mweleko wasijue la kufanya baada ya kuangukiwa na ukuta wa nyumba yao ya tope.

"Licha ya kuwa na maumivu ya kifua Nyonga ninaendelea vizuri nawashukuru madaktari walionisadia mimi na mke wangu,” amesema John.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwabasabi B Kijiji, Dotto Msula amesema baada kusikia kishindo alitoka nje na kukuta nyumba ya jirani yake imedondoka ndipo alipochukuwa jukumu la kuwaokoa, huku alipiga kelele wananchi walijaa na kufanikisha kuwaondoa kwenye kifusi.

"Baada ya kuwaokoa tulichukuwa pikipiki na kuwakimbiza Hospitali kwa ajili ya matibabu na kwa mjibu wa dakitari baada ya kuwa hudumia hali zao zinaendelea vizuri,” amesema Msula.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyamazugo Enock Sengerema ambaye amefika Hospitalini hapo kuwajulia hali majeruhi amewashukuru madaktari waliowahudumia kuonyesha moyo wa upendo.

Amesema kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa hapa nchini nyumba nyingi ambazo siyo imara zitaendelea kudodoka hivyo wananchi wanatakiwa kuchukuwa tahadhari juu hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live