Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa mbaroni kwa uhujumu Uchumi

MBARONI.jpeg Wanandoa mbaroni kwa uhujumu Uchumi

Wed, 22 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanandoa Benedict Masasi (36) na Faraja Sago (31) wakazi wa mtaa wa Mjimwema mjini Njombe wamefikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi Njombe wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa makosa matatu ikiwemo kuuza mbolea feki iliyowekwa kwenye mifuko 221 na kuuzwa kwa wakulima zaidi ya 58 na kuisababishia hasara Mamlaka ya Udhibiti wa Mbokea Tanzania (TFRA) kiasi cha Tsh Milioni 26,288,794.

Wakisomewa mashtaka hayo na wakili wa serikali kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka mkoa wa Njombe Matiku Nyangero amesema kosa la kwanza walilotenda ni kuuza mbolea feki kinyume na kifungu cha sheria cha 40 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili cha sheria ya mbolea ya mwaka 2009 na kosa la pili ikiwa ni kula njama ya kutenda kosa kinyume na kanuni ya paragraph ya 4 kifungu cha kwanza cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 marejeo ya 2022 huku kosa la tatu ikiwa ni kuisababishia hasara mamlaka ya kudhibiti mbolea Tanzania kinyume na kanuni ya paragraph ya 10 kifungu cha kwanza ya jedwali la kwanza la kifungu cha 57 na 60 cha sheria ya uhujumu uchumi sura ya 200 iliyofanyiwa marejeo mwaka mwaka 2022.

Nyangero amesema makosa hayo yalitendeka kati ya mwezi Novemba mwaka 2022 hadi January 2023 maeneo ya mitaa ya Mgodechi na Ramadhani ndani ya wilaya na mkoa wa Njombe ambapo pia imeelezwa kuwa wastakiwa walikuwa wakiuza mbolea za ruzuku zilizopunguzwa ujazo.

Hakimu mkazi wa Mahakama ya mkoa wa Njombe Lihad Chamshama amesema kuwa washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na malaka ya kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Aidha washtakiwa hao wametakiwa kuweka bondi ya shilingi milioni 30 ya mali zisizohamishika ambapo wao wawiwili wameweka bondi ya shilingi milioni kumi kila mmoja na wadhamini wao wawili wameweka dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja na wako nje kwa dhamana kwa mujibu wa wa sheria kifungu cha 29 kifungu cha 4 cha makosa ya uhujumu uchumi na wamepewa dhamana mpaka hapo march 30 mwaka huu kesi itakapo tajwa tena.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live