Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanandoa ambao hawaoni,jinsi wanavyoishi "niliibiwa mke na rafiki yangu,mke hanijui"

Video Archive
Tue, 25 May 2021 Chanzo: millardayo.com

Rashid Abrahaman ni kijana ambaye alipata tatizo la kutokuona baada yakuugua wakati anahangaika kutafuta dawa rafiki yake alimpa dawa ambayo ilipelekea kutokuona kwa kuwa macho yake yaligeuka nje ndani nakupelekea kutokuona hadi leo baada yakupambana hospitalini kwa muda mrefu bila kupata matibabu kutokana nakukosa fedha.

Rashidi anasema alioa mwanamke aliyezaa naye watoto wawili ambaye baadaye alikuja kuchukuliwa na rafiki yake ambaye alikuwa jirani yake nakuzaa naye mtoto mmoja lakini alikutana na Mariam ambaye na yeye alikuwa haoni ambapo hadi sasa wanaishi pamoja baada yakufunga ndoa mwaka mmoja uliopita.

“Mke wangu wa kwanza aliolewa na rafiki yangu akaenda kuzaa naye mtoto kwa kuwa sikuwa na fedha kwa kuwa nilikuwa nafanya kazi kijiweni na walikuwa wanakuja kufanya matumizi karibu yangu,huyu mke wangu wote hatuoni na tunaishi pamoja ila hatuna hela yakulipa kodi na tunaishi kwenye chumba kimoja na watoto”-Rashid

Chanzo: millardayo.com