Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wavamia gali la mafuta lililopata ajali, wakimbizana kuchota!-VIDEO

Mafuta Yaibwa Wananchi wavamia gali la mafuta lililopata ajali, wakimbizana kuchota!

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya Watanzania ni kama hawajifunzi!

Unalikumbuka tukio la takribani watu 71 kufariki dunia mwaka 2019, Msamvu mkoani Morogoro baada ya kuchota mafuta ya petroli kwenye eneo la ajali kisha moto kulipuka?

Basi hilo halikuwa funzo kwa baadhi ya watu, kwani tabia hiyo inaendelea.

Katika tukio jipya, baadhi ya wananchi wa Handeni mkoani Tanga, wameonekana wakichota mafuta kwenye eneo la ajali baada ya lori kupinduka katika eneo la Segera mkoani humo.

Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, @smchembe amelipongeza jeshi la polisi kwa kuwadhibiti wananchi wa Kata ya Segera ambao walivamia gari la mafuta lililoanguka na kuanza kuchota petroli.

View this post on Instagram

A post shared by Tanzania Web (@tanzaniaweb)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live