Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi watumia viroba vya taka kufunga barabara

29817 TAKA+PIC TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni.  Leo Jumapili Desemba 2, 2018 kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 watu wanaotumia barabara inayotoka Skanda kwenda Mahakama ya Mwanzo hadi Msikiti Mkuu katika halmashauri ya mji wa Handeni, jijini Tanga wamelazimika kutafuta barabara nyingine kufuatia barabara hiyo kufungwa na watu wasiojulikana.

Wakizungumza na Mwananchi kuhusu barabara hiyo iliyokuwa imezibwa kwa viroba vya taka, baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wamesema jana hazikuwepo, wamezikuta leo asubuhi.

Mfanyabiashara Robert Kamoga amesema taka hizo zimekuwa ni kero kwao kwa maelezo kuwa baadhi ya wateja hawafiki kwenye biashara zao kutokana na taka hizo, baadhi ya watu wameamua kuziweka barabarani ili kutuma salamu kwa mamlaka husika zenye jukumu la kusomba taka hizo.

“Halmashauri ilitangaza watu watoe takataka ili gari liweze  kuzizoa ila gari halijaonekana hivyo kuna wananchi wameamua kuziweka barabarani ili Serikali ione wamekereka,” amesema mfanyabiashara huyo.

Diwani wa kata ya Chanika,  Abdallah Chihumpu na baadhi ya viongozi walifika eneo la tukio na kuzungumza na wafanyabiashara hao na kukubaliana kuziondoa taka hizo na utaratibu wa kuzizoa utaendelea kama kawaida.

Wiki iliyopita wafanyabiashara walimuomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuchukua hatua za kuwatafutia eneo maalum la kuweka takataka kutokana na sehemu inayowekwa taka kuonekana sio sahihi kwa kuwa lipo katikati ya mji. 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz