Wananachi wa Kijiji cha Nyamikoma kilichopo Wilayani Butiama mkoani Mara wametishia kuchoma moto kijiji hicho endapo Mtendaji wa kijiji hicho Goodluck Makunja atahamishwa ambapo wanadai amekuwa akitenda kazi kiudalifu tofauti na watendaji waliopita.
Wananchi hao wamefikisha ombi hilo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Patricia Kabaka baada ya kupata taarifa ya kuhamishwa kwa mtendaji huyo kijijini hapo.
Katika mkutano wa dharura uliofanyika katika kijiji hicho ajenda ilikuwa moja tu ya kutaka mkurugenzi kusitisha uamauzi wake wa kumwamisha mtendaji huyo wa kijiji.
Wanachi hao pia walibeba mabango yenye maandishi tofauti tofauti ambayo yalikuwa yakimtaka mkurugenzi huyo kubadili maamuzi ya kumwamisha mtendaji huyo wa kijiji na hapa wanaelezea hisia zao.
Mkurugenzi wa Halmashauri akizungumzia suala hilo kwa njia ya simu amesema hakuna jambo lililofichwa juu ya suala hilo ila ni taratibu za kazi ambapo kila mtumishi anaweza kuhamishwa.