Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wataka kuundwa tume mgogoro wa ardhi, Nyasa

Ziwani.png Sehemu ya eneo la marufuku, Nyasa

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mahanje halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume maalum ikachunguze mgogoro uliopo baina yao na mamlaka ya bonde la ziwa Nyasa.

Wakazi hao ambao ni wakulima wa mazao mbali mbali ikiwemo Mahindi,Maharagwe,Ndizi na mazao mengi mchanganyiko wanasema mgogoro wao mkubwa na mamlaka hiyo ni kutokana na kuzuiwa kuingia na kuendeleza kilimo katika eneo la zaidi ya ekari 400 walilokuwa wakilitumia miaka yote ikidaiwa kuwa ni sehemu ya hifadhi ya vyanzo vya maji Namahove.

Wakazi hao akiwemo Christian Ngonyani,Joseph Chipeta na Joyce Mvula wanasema kwa sasa wamekuwa ni wahanga wakubwa katika maeneo yao hali inayowasababishia baa la njaa kutokana na kukosa maeneo ya kulima.

“Nimenyang’anywa maeneo katika eneo la kibandisi mpaka sasa hatuna eneo la kulima,tunashinda njaa na maisha yamekuwa ni magumu tunaomba mama Samia utusaidie kwa kuwa tumewekewa vibao na kuambiwa ni marufuku kuingia kwenye eneo hili”alisema Joyce Mvula

Joyce Chipeta alisema “Kutoka kwenye mlima kule mpaka hapa tulipo ni zaidi ya kilomita mbili ambako ndipo yalipo mashamba ya watu na kitendo kilichofanyika hakijafanyikia kwa uhalali kwasababu haujafanyika ushirikishwaji”

Diwani wa kata ya Mahanje bwana Stephano Mahundi anasema baadhi ya mikutano ilifanyika ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya mchakato uliofanyika lakini wananchi wa kijiji hicho wameona wameona utaratibu uliofanyika haukuwa sawa.

“Kwa Mahanje watu walifikiri kauli ile ya mita 60 ndio maeneo ambayo yatachukuliwa lakini kilichotokea sasa baada ya kuweka mipaka wananchi wameona ni tofauti na kile ambacho walifikiri”alisema Mahundi

Bi,Elice Engelbert ni mkurugenzi wa bodi ya bonde la ziwa Nyasa,amekili juu ya kuweka mipaka hiyo huku akibainisha kuwa vikao kadhaa na wananchi vimefanyika juu utunzaji wa eneo hilo mpaka kuweka mipaka huku akishangazwa na malalamiko ya wananchi hao na kuongeza kuwa eneo hilo limekuwa na migogoro pia ya mipaka.

“Watanzania wanajua chanzo cha maji ni pale maji yanapotokea tu,sio hivyo tu ila ni kuanzia pale ambapo maji yanatoka,yanatiririka mapaka yanapoishia.lakini sasa unaweza kukuta maeneo mengi ambayo mito mingi inaingia haya maeneo hayawezi kuwa sawa na utakuta kuna maeneo bikoni imekaa mbali na sehemu nyingine imeingia ndani kutokana na kipimo”alisema Bi,Elice

“Sheria ya mazingira inasema mita 60 lakini kuna sheria ya rasilimali za maji inakwenda zaidi ya mita 60 kwa eneo ambalo ni la maji na umuhimu wa hicho chanzo na hicho ndicho kipaumbele kwa hiyo eneo la chnazo linakwenda zaidi ya hapo na tulichokifanya Mahanje bado hatujachukua maeneo yote”aliongeza

Aidha Bi,Elice Engelbert amesema msimamo wa bodi ya maji bonde la ziwa Nyasa ni kuendelea kusimamia kikamilifu eneo hilo na kuagiza wananchi kutoingilia maamuzi juu ya eneo hilo na wapo tayari kuchukua hatua ya kisheria kwa mwananchi atakayekaidi maelekezo ya bodi kwa kuwa walikwisha toa maelekezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live