Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wataka kurejeshewa fedha zao uvuvi

Pic Fedha Data Wastaafu Wananchi wataka kurejeshewa fedha zao uvuvi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika mto katuma ambao unadaiwa kuwa ndani ya hifadhi ya Katavi wameomba kurudishiwa fedha waliotoa kwaajili ya kukatiwa vibali vya uvuvi kutokana na vibali hivyo kutoainisha eneo la kufanyia shughuli hiyo.

Madai hayo yamekuja baada ya Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph kufika katika eneo la Sitalike na kusikiliza kero za wakazi wa eneo hilo na kubaini wananchi hao kukosa eneo la kuvulia samaki haliyakuwa wanavibali vya kufanya shughuli hiyo.

Akijibu hoja hiyo Afisa kilimo, mifugo na uvuvi halmashauri ya Nsimbo Daniel Walakunga amesema kibali walichopewa kiliwaelekeza kufanya shughuli za uvuvi eneo lolote ambalo halipondani ya hifadhi huku Afisa Uhifadhi Meleji Mollel akidai shughuli za uvuvi katika mto katuma zilizuiliwa kutokana na baadhi ya watu kutumia mwanya huo kufanya uhalifu ndani ya hifadhi.

Nae Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ameagiza wananchi hao kurudishiwa fedha yao ili kuepusha mgogoro ambao siowalazima baina ya wananchi na serikali.

Mbali na kero hiyo pia wananchi hao wameomba kuboreshewa miundombinu ya afya katika zahanati ya Sitalike hususa ni jengo la huduma za kina mama wajawazito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live