Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi washauri watoto wasilazwe na wageni

Wazzazii Baadhi ya wananchi wa Kata ya Goba

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwalaza watoto wao chumba kimoja na wageni wanaofika majumbani mwao bila kujua undani wa tabia zao imetajwa kuchangia kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na ulawiti kwa watoto kutokana na wengi wao kurubuniwa kwa vijizawadi kama vile pipi, soda na biskuti

ili wasiwaambie wazazi wao na kisha kuingiliwa kingono, hali ambayo imekua ikihatarisha kuongezeka kwa vizazi visivyo na maadili katika jamii nyingi hapa nchini. 

Wakizungumza na EATV wazazi wa Matosa, Kata ya Goba wilayani Ubungo wamesema tabia ya baadhi ya familia kuwalaza watoto wao na wageni iwe wa kike au wa kiume imekua sababu kubwa inayochangia kuongezeka kwa matukio ya ubakaji na ulawiti kwani wengi wao hutumia mbinu chafu za kuwalaghai kwa zawadi na hivyo kuwaingilia hatua ambayo wamesema imekua ikihatarisha ukuaji wa watoto wadogo.

Wakielezea namna ya kukabiliana na changamoto hizo mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika mtaa wa Matosa Halisi Sophia Ndawale, wamesema ipo haja ya wazazi, walezi na jamii kiujumla kuhakikisha wanajenga urafiki na watoto wao ili kupata taarifa za siri juu ya matukio hayo ili sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live