Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waomba ulinzi kutokana na wanawake wanaojiuza

Pembe Web Wananchi waomba ulinzi kutokana na wanawake wanaojiuza, uhalifu

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa linawashikilia watu watatu walijiohusisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokea Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya huku wananchi wakiomba polisi kuimarisha doria kufuatia kuwepo kwa kundi la wahalifu hususani wanawake wanaofanya biashara za kujiuza.

Mkazi wa Forest, jijini Mbeya ameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha doria katika maeneo ya Mataa kufuatia kuwepo kwa kundi la wahalifu hususani wanawake wanaofanya biashara za kujiuza na kuleta kero kubwa kwa watembea kwa miguu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga ameiambia Mwananchi Digital leo Jumapili, Septemba 17,2023 kuwa tukio la kwanza mkazi wa kijiji cha umalilo Usongwe Wilaya ya Mbeya, Seleman Ezekiel (34) anashikiliwa kwa tuhuma za kupatikana na meno ya tembo yenye uzito wa gram 7.5.

Kuzaga amesema wakazi wawili wa Ipogoro Mkoa wa Iringa, Sylivester Raphael (34) na Shukuru Mlowe (35) wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na utapeli wa mitandao ya simu za mkononi.

Watuhumiwa hao walikamatwa katika Kata ya Igawa Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya na kwamba walikuwa wakisakwa katika Mikoa ya Mbeya Iringa, Dodoma na Njombe ambako waliruka dhamana ya polisi baada ya kushtakiwa kwa kesi ya utapeli.

Tukio la pili amesema mtuhumiwa alikamatwa katika kijiji cha Malunda Wilaya Mbarali Mkoa wa Mbeya baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na hifadhi ya Taifa (Tanapa) walipokuwa kwenye doria walimtilia shaka na kisha kulazimika kumfanyia ukaguzi kwenye mfuko aliokuwa ameubeba.

“Walimtilia shaka mtuhumiwa kwenye mfuko wa sandarusi aliokuwa ameubeba baada ya kumfanyia upekuzi walibaini kuwepo kwa meno ya tembo mawili yenye uzito wa gram 7.5,” amesema Kuzaga.

“Nitoe onyo kwa wahalifu watambue kuwa Mkoa wa Mbeya tumejipanga yoyote atakaye jihusisha matukio ya uhalifu lazima abainike na kuwataka kufanya kazi za kujitafutia riziki kihalali,” amesema.

Kuzaga amesema watuhumiwa bado wanaendelea kuhojiwa na polisi mara baada ya uchunguzi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live