Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wamzomea Mkurugenzi Kahama

Makondaaa 096979 Wananchi wamzomea Mkurugenzi Kahama

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wamemzome Mkurugenzi wa Manispaa Kahama, Anderson Msumba na Ofisa Mipango Miji wa Manispaa hiyo, Clemence Mkusa, kwa madai ya kuchochea migogoro na kupewa majibu mabaya.

Tukio hilo limejitokeza jana wakati wa mkutano wa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, alipokuwa anasikiliza kero za wananchi  ambapo walieleza kutokuwa na imani na viongozi hao.

"Makonda ukiondoka, Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa anatusikiliza  vizuri na wanatoa maamuzi lakini Mkurugenzi ndio chachu ya migogoro anagoma kutusikiliza na maofisa ardhi lakini kikubwa ni Mkurugenzi.

Mkuu wa Wilaya ameagiza nipimiwe maeneo yangu lakini Mkurugenzi hataki anadai kasomea sheria na hafuati mambo ya siasa, " alisema Caroline Magige ambaye ni mkazi wa Wilaya hiyo. 

Calorine alimueleza Makonda hata akiwasikiliza kero zao nani atazitekeleza" huyu Mkurugenzi ni chanzo cha migogoro nimeangaika leo ni mwaka wa kumi naangaika na kesi, Waziri mwezi uliopita katoa maelekezo kuwaambia huyu mama sio mvamizi naomba apatiwe maeneo yake na kama hayapo aelezwe yameenda wapi mpaka leo ni kimya hakuna utekelezaji, "

Chanzo: www.tanzaniaweb.live