Serengeti. Wakazi wa Robanda wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara wametoa ng'ombe wawili kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla.
Ng’ombe hao wametolewa leo Jumanne Juni 18,2019 na Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Mrobanda Japani kwa viongozi hao kutokana na utendaji wao wakati wa hafla ya kutambulisha tuzo ya ubora wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa wakazi wa mikoa ya Mara na Simiyu.
Japani ameomba Waziri Kigwangalla kuhakikisha timu iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia migogoro ya wananchi na wahifadhi iweze kufika kijijini hicho kumaliza migogoro hiyo kabla ya uchaguzi.
"Naomba wafanye kabla ya uchaguzi ili isije kuwa ni kisingizio cha kukosa kura," amesema.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dk Kigwangalla amesema wizara hiyo imeanza kupitia kanuni za ulipaji kifuta machozi na jasho kwa watu wanaouawa, jeruhiwa na mazao kuliwa na wanyama.
"Wataalam katika wizara wanaendelea na mchakato huo na pia ulipaji wake utakuwa unafanyika kwa wakati,” amesema.
Pia Soma
- Benki ya PBZ kufunga ATM 14 Z’bar, Dar
- Watumishi saba wa Nida mbaroni
- Takukuru yawasaka wamiliki kampuni ya Meis Industriesltd kwa kurokoka na Sh46 bilioni
Kwa mjibu wa kanuni ya ulipaji fidia ya mwaka 2011 ekari moja inalipwa kati ya Sh100,000 na mtu akiawa analipwa Sh1 milioni.