Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wamkataa Diwani mchana kweupe!

Diwani Mchan.jpeg Wananchi wamkataa Diwani mchana kweupe!

Sat, 3 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Muwimbi kata ya Lumuli, wilayani Iringa wameamua wampinga Diwani wao Muwimbi Mlusi kwa utendaji usioridhisha huku wakidai kuwa katika kipindi chake cha uongozi, kata hiyo imerudi nyuma kimaendeleo.

Hata hivyo Diwani huyo, ameiambia Mwananchi Digital kuwa madai yote yanayoelekezwa kwake siyo ya yakweli na kwamba ni kikundi kidogo cha watu wachache wanaotaka kumchafua na kumharibia rekodi yake ya utumishi uliotukuka. Aliongeza kwa kusema kuwa yupo nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kama waandishi wa habari wanaotaka kujua undani wa taarifa hizo basi wamsubiri mpaka atakapoitishisha mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine, atazungumzia jambo hilo.

“Najua ni kikundi kidogo tu cha watu ambacho kinawadanganya na kuwapa taarifa ambazo si za kweli lakini na mimi najua kila kitu kilichoendelea kijiji na niliwaona toka mnafika nikakaa tu sehemu sikutaka kuongea chochote mpaka mnaondoka natambua kila kitu,” alisema Mlusi. Diwani huyo aliongeza kwa kusema kitendo cha waandishi wa habari kufika katika kijijini kwake bila kutoa taarifa kwa kiongozi ni jambo bamya na kwamba hajapendezwa nalo. Awali wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao wamesema kuwa hawakubali kuendelea kuona Diwani akifanya kazi tofauti na matakwa yao. Pia wamelalamikia kitendo cha diwani huyo kutoa kazi ya ufyatuaji wa matofali na kujenga shule bila malipo kufanyika kitu ambacho kinayumbisha uchumi wa kazi zao. "Tunawaomba viongozi mbalimbali wa ngazi za juu kama wanatusikia waweze kufanya kitu chochote kwani muda mrefu tumekua tukivumilia uongozi huu ila kwa sasa tunaomba msaada,” alisema mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka kujitambulisha. Lakini kwa upande wa James Ndongolo, yeye analalamika kitendo cha Diwani huyo kuzichukua tofari hizo bila ya kuwalipa na kwamba inaonekana ni kana kwamba aliwatumia kwa maslahi yake binafsi huku akiwaacha wakisononeka. "Malipo ya matofali hayo yalifanyika kwa kiasi kidogo na kiasi kingine mpaka leo bado mgogoro, Mimi naomba viongozi mnaonisikia mnisaidie fedha iliyobakia ni Sh295000," alisema Ndongolo na kuongeza; "Sisi ni vijana ambao tunahangaika kila siku ili tupate kujikwamua kimaisha magumu kijijini hapa lakini sasa kwa hali hii ni ngumu, tunajikuta tunashindwa.” Nae Richard Ndalilwe alisema kuwa mateso mengi waliyopitia katika uongozi wa Diwani huyo itoshe kuachwa sasa waishi kwa amani katika kijiji chao kwa kufanyiwa maendeleo mbalimbali yanayohitajika na Wananchi kwani wamevumilia mengi ikiwemo mara kwa mara kuona mapungufu katika baadhi ya maeneo japokuwa kiongozi anapoulizwa hujibu majibu yasiyo ridhisha. “Mfano katika mkutano wa hadhara uliopita nilimuuliza Diwani, Je kuna pesa za vikundi vya vikoba mpaka leo hatujaona maendeleo yake, lakini Diwani alivyonijibu ni kwamba masuala ya pesa za vikoba ningenifuata huko kwenye vikoba na sio pale," amesmea Ndalilwe Hata hivyo Ndalilwe anaamini kuwa kwenye mikutano ya hadhara ndiko sehemu sahihi kwa wananchi kutoa dukuduku zao na hasa kwa mambo yanayohusi kijiji chao na kwamba kitendo cha kuzuiwa ni kinyume na utaratibu. Naye Fredy Mtende Mjumbe wa Halmashauri ya kijiji cha Lumuli alisema ni kweli uongozi wa Diwani haupo sahihi na kuna makosa mengi mfano ni saruji za kujengea bweni la shule ya Sekondari Lumuli ambapo mzigo huo ulihamishwa kijijini hapo na kupelekwa Mafinga na kwamba anapoulizwa hutoa majibu yasiyoridhisha. "Tumekuwa tukiona akitembelea wawekezaji kijijini hapa tena akiwa mwenyewe, tukimuuliza kwanini unaenda pake yako, majibu yake huwa siyo ya kuridhisha akisema kama ni suala la kuomba ufadhili, lazima aende yeye kama yeye,” amesema Mtende

Chanzo: www.tanzaniaweb.live