Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi walipwa mabilioni kupisha mradi wa madini

Fri, 18 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Takribani wananchi 776 wa vijiji saba vilivyopo kata ya Matambale wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi  wamelipwa Sh7.45bilioni za  fidia ya mazao yao ili kupisha mradi wa uchimbaji madini.

Hayo yamebainishwa leo Alhamisi Januari 17, 2019 na msemaji wa kampuni ya Urenix,  Alley Mwakibole wakati akizungumza na Mwananchi ofisini kwake.

Amesema mradi wa uchimbaji na utengenezaji bidhaa zinazotokana na madini ya Bunyu Grafite utaanza hivi karibuni baada ya kukamilika kwa ulipaji fidia ya ardhi na mazao kwa wananchi wa vijiji vya Matambarale Kusini, Matambarale Kaskazini, Chiundu, Chunyu, Mihewe, Namkatila na Namikulo

Amesema katika mradi  huo watu 776 waliopisha mradi kati 785 wamelipwa kiasi hicho cha fedha, kwamba ambao hawajalipwa waligoma kiwango walichopewa kuwa ni kidogo.

Amesema mradi huo unatarajiwa kuajiri watu zaidi ya 400 na kati yao  59 wa watajengewa nyumba za makazi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi  amesema Serikali inatambua umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya wananchi wa Mkoa huo.

Amesema wananchi wakitumia fursa hiyo vizuri itawakomboa kwa kuwa watajipatia ajira.

Subira Hamisi, mkazi wa Nachunyu amesema kuanza kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana wilayani Ruangwa na mkoani Lindi.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz