Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi walia visima vyao kujazaa mawe

Screenshot 20230715 205022 Facebook Wananchi walia visima vyao kujazaa mawe

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Visima vitatu vya maji katika Kijiji cha Lembapuli Kiteto vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 100 vimejazwa mawe na watu wasiojulikana

Akizungumza mbele ya Mbunge wa Jimbo la Kiteto diwani wa kata ya Loolera Kosei Lehinga amesema Kijiji cha Lembapuli mpakani mwa Kiteto na Kilindi ya Tanga kuna mgogoro wa mipaka uliodumu muda mrefu bila ufumbuzi ambapo hata gari la mtu binafsi liliwahi kuchomwa moto

Amesema visima vitatu vilivyochimbwa na wananchi wa eneo hilo ili kusaidia maji ya mifugo na binadamu kwa nyakati tofauti vimekuwa vikijazwa mawe na watu wasiojulikana ambapo wamemuomba mbunge kuingilia kati

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lembapuli Ole Lekaita ameagiza ufanyike uchunguzi wa haraka kwa nia ya kuwasaidia wananchi hao ambao juhudi zao zinafifishwa huku akisema nia ya Serikali ni njema na kutaka wakamatwe na kufikishwa kwenye mikono ya sheria wanao hujumu miradi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live