Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi walia maji kuweka matatani ndoa zao

MAJII Wananchi walia maji kuweka matatani ndoa zao

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi zaidi ya 3,000 wanaoishi katika kijiji na Kata ya Kimambi, wilayani Liwale, mkoani Lindi, wanaiomba Serikali kuwaongezea tanki lingine la maji, kwani lililopo halikidhi mahitaji yao, huyu yaliyopo ni ya chumvi ambayo wanadai hayafai kwa matumizi ya kunywa.

Wakizungumza na Mwananchi Digital leo Ijumaa Oktoba 20, 2023, wakazi hao wamesema kuwa wanalazimika kutembea zaidi ya kilometa 5 usiku wa manane kufuata maji na hivyo kujikuta wakiweka uhai pamoja ndoa zao hatarini.

Hawa Shaweji ambaye ni Mkazi wa Kata ya Kimambi, amesema kuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya kilometa 5 kufuata ya maji ya chemichemi katika eneo la Njengani na amesema kuwa wakati wakwenda kuchota maji wanakutana na wanyama wakali kama tembo ambao wanahatarisha maisha yao.

"Natoka nyumbani saa tisa usiku kwenda kuchota maji, kurudi hadi saa 8 mchana hivi mwanaume gani anaweza kuvumilia hali hiyo, tunagombana na wanaume zetu kila wakati, mimi niiombe Serikali itupatie tanki la maji lililokubwa na lenye maji salama kama yale ya chemichemi ilikutuondolea adha hii,” amesema Hawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live