Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi walalamikia foleni zoezi ugawaji wa mahindi

Maguni Ya Mahindi Wananchi walalamikia foleni zoezi ugawaji wa mahindi

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanakijiji Tanga wanapanga foleni kupata msaada wa mahindi na pia lazima waje na vitambulisho, wanauziwa kilo moja kwa shilingi mia tisa, watu ni wengi sana na foleni huenda ikawa hadi jioni na kitu endelevu.

Kinachofanyika kwa sasa kimekuwa kikifanyika wiki nzima yote hii. Wanaunganika wanavijiji wa Handeni kupata huduma huu, kinachosikitisha zaidi ni kuwa mtu anaweza kumaliza saa kadhaa kukaa kwenye foleni.

Wao wanasema ni mahindi ya msaada lakini kwamba kuna mtu kajitolea kuwapa lakini masharti ya kuyapata ni mengi na lazima uwe na utambulisho wa Kijiji ndio unahudumiwa.

Mkuu wa Wilaya aelezea Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe anasema: “Kwa mujibu wa tafiti iliyofanywa na wenzetu wa World Vision wakishirikiana na Wizara waliona kuna kata zina upungufu wa chakula, changamoto ambayo imetokana na ukame wa mvua katika maeneo mengi.

“Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na changamoto hiyo aliamua kutupatia msaada wa chakula tani 100 za mahindi ya bei nafuu, tukagawa yakaisha.

“Jana (Novemba 23, 2022) tulipokea mahindi mengine tani 100, hayo yanauzwa ambapo mwananchi anakuwa ameokoa Tsh. 420 kwa kila kilo moja, zoezi la ugawaji linaendelea hadi sasa.

“Kuhusu madai ya kuwepo kwa foleni kubwa na utaratibu mwingine wa ugawaji chakula naomba wanaojua hilo ni NFRA (Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula), wao ndio wanaoweza kutoa taarifa rasmi.”

Ufafanuzi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Valeria Mwenda wa NFRA anasema: “Kwa siku nawapimia watu hadi 150, anayepokea chini zaidi ni anayepokea kilo mbili, natumia mkono kupima, foleni ipo lakini sidhani kama kuna mtu ambaye anaweza kukaa kwa saa kadhaa.

“Changamoto iliyopo hapa, watu hatupeani ushirikiano, kila mtu akija anataka kuwa wa kwanza, mwisho wa idadi ya kilo kw amtu mmoja ni kilo 100, wengine wanataka zaidi ya kilo 100 ukiwakatalia wanalalamika.

“Hapa hatutuo mahindi kwa ajili ya kwenda kuuzwa bali kwenda kutumiwa na wananchi, hivyo kuna wengine wanaokuja kwa lengo la kuchukua mahindi ya biashara, wakikwama ndio wanalalamika.

“Hapa kwa siku napima hadi tani 19 kwa siku, natumia mkono, naweza kujiuliza hiyo kazi ni kubwa kiasi gani.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live