Baadhi wa Wanandoa katika Kijiji cha Igawa, kilichopo Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro wameingi katika migogoro ya kifamilia inayopelekea ndoa kuvunjika, baaada ya mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, kudaiwa kugeuka popobawa na kufanya mapenzi na wake za watu nyakati za usiku.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wa Kijiji hicho wamesema mtu huyo amekua akivunja uhusiano wa wanandoa kwa wanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa na wenzi wao wanaodai kutojisikia kufanya hivyo baada ya kujikikuta wameingiliwa kimapenzi kwa njia za kishirikina.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mathew Massele amefika katika kijiji hicho na kuzungumza na wanachi ambapo amewataka waache imani za kishirikina huku akisisitiza kua huyo ni mtu kama watu wengine na tayari Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.
Amesema, “Nimepita kituo cha Polisi kumuangalia huyo mtu mnaemwita popobawa nikajua kitakua kitu cha ajabu kumbe ni binadamu tu, ndugu zangu acheni imani za kishirikina huyu ni mtu kama mlivyo ninyi acheni kumsingiza mambo ya hovyo.”
Hata hivyo, Massele ameongeza kuwa, “Mkiendekeza imani za kishirikina mtasababisha uvunjifu wa amani hivyo masuala hayo hayapaswi kupewa kipaumbele katika masisha yenu.”