Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi walalamika kutumia maji ya madimbwi na wanyama

Shy Wananchi walalamika kutumia maji ya madimbwi na wanyama

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Wananchi wa Kijiji cha Mwaningi Kata ya Bulige Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamelalamika kutumia maji machafu huku wakichangia na wanyama jambo ambalo wanadai linahatarisha afya zao.

Wakati wakilalamikia hali hiyo, mkandarasi ambaye anatekeleza mradi wa maji kijijini humo anadaiwa kuutelekeza.

Wametoa malalamiko hayo mbele ya Naibu Katibu Mkuu wa maji Cyprian Luhemeja, alipofanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji kwa wananchi mkoani humo.

Malita Charles mkazi wa kijiji hicho amesema wanakabiliwa uhaba mkubwa wa majisafi na salama na wamekuwa wakitumia maji ya kwenye mabwawa kwa matumizi yote ya nyumbani.

“Tunaomba kiongozi wetu utusaidie maji haya ni machafu kwelikweli tunakunywa na tunakunywa na fisi kabisa pamoja na wanyama wengine hawa wanyama ni hatari,”amesema

Mkazi mwingine Modesta Masai amesema matumizi ya maji hayo yamekuwa yakihatarisha afya zao na hata kupata magonjwa ya matumbo ya mara kwa mara.

Kutokana na hali hiyo, Naibu Katibu Mkuu Luhemeja ameagiza Mkandarasi ambaye ametelekeza mradi wa maji kutoka Kampuni ya Pet Cooperation Limited kuripoti kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

“Muongozo wa Wizara unasema kampuni ambayo yanashindwa kufanya kazi yafutwe kabisa na hii kampuni ni moja wapo liwekwe kwenye ‘Black List’ sababu lengo kuu la Serikali kutumia Wakandarasi kutekeleza haraka miradi hii ya maji ikamilike haraka, lakini huyo ameleta dharau,” amesema Luhemeja

Pia amemuagiza Meneja Wakala wa Maji Safi na usafi wa Mazingira vijijini (Ruwasa) Mkoa wa Shinyanga, Julieth Payovela, kwamba fedha ambazo atazirudisha mkandarasi huyo wapewe wananchi wa kijiji hicho wachimbe mitaro ya mabomba hadi kufika Oktoba uwe umakamilika kwa kutumia Force Account.

Naye Meneja wa Ruwasa, Payovela amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Februari mwaka jana na ulitakiwa kukamilika Juni mwaka huu kwa gharama ya Sh2.2 bilioni lakini mkandarasi huyo ameutelekeza akiwa ameshachukua baadhi ya fedha.

Chanzo: Mwananchi