Wananchi wa vijiji vinavyotegemea kupata huduma za afya katika kituo cha afya Ifwagi, halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wanapitia katika wakati mgumu kutokana na kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye kituo hicho jambo linalowalazimu mgonjwa anapofariki kubeba maiti na kwenda kuifungia nyumbani huku wakitakiwa kutolia na kusababishi kadhia kubwa kisaikolojia.
Akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Ifwagi Naibu Waziri wa Viwanda ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo Exaud Kigahe, ameguswa na changamoto hiyo na kutoa maelezo kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi.
#VIDEO Wananchi wa vijiji vinavyotegemea kupata huduma za afya katika kituo cha afya Ifwagi, halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wanapitia katika wakati mgumu kutokana na kukosekana kwa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye kituo hicho jambo linalowalazimu mgonjwa… pic.twitter.com/dXn4SS6PMk
— EastAfricaTV (@eastafricatv) March 11, 2024