Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wakosa maji,yaelekezwa kwa muwekezaji

MOLLEL Wananchi wakosa maji,yaelekezwa kwa muwekezaji

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: Eatv

Mkuu wa wilaya ya Siha Dkt.Christopher D.Timbuka na mbunge wa Siha Dr Godwin Mollel wamebaini kutopatikana kwa maji katika eneo hilo kwa muda mrefu kumesababishwa na  hujuma ambazo zinafanywa  na kiongozi wa Bonde la Pangani akishirikiana na wawekezaji wanaomwagilia shamba la Parachcichi.

Hayo yamebainishwa hii leo na viongozi hao baada ya kufanya ziara ya kukagua vyanzo vya maji ambavyo hutumika kupeleka maji katika jimbo hilo na kusema kuwa wamekuwa wakifunga maji na kuelekeza upande wa muwekezaji jambo ambalo limeleta athari kubwa kiuchumi na kijamii 

“Amefungia maji yasishuke chini na kusababisha athari mbalimbali wanachi kukosa maji,wanyama wanaopatikana katika maeneo yam lima Kilimanjaro nao wanakosa maji na kuathiri sekta ya utalii pia”alisema Dr Mollel.

Hata hivyo Kiongozi wa bonde hilo Mhandisi Segule amekiri wazi kuwa, mwekezaji anapewa maji lita 130 kwa sekunde, huku wananchi wakipewa lita 20 kwa sekunde na mazingira yakipata sifuri.  

Chanzo: Eatv