Dar es Salaam. Mamia ya wananchi na wanachama wa CCM wamejitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) katika hafla fupi ya kupokea ndege ya pili ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania.
Ndege hiyo imewasili leo saa 8:36 mchana ikitokea nchini Marekani na kupokewa na Rais wa Tanzania, John Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Spika wa Bunge, Job Ndugai, mawaziri, wakuu wa mikoa na mabalozi.
Wakizungumzia ujio wa ndege hiyo, wananchi hao wamesema ndege hizo ni chachu ya kuongeza mapato ya Serikali.
"Nimefurahi sana kununuliwa kwa ndege hizi, zitasaidia kuboresha usafiri. Sasa wageni wengi watakuja nchini kwa ajili ya utalii,” amesema Henry Kissu, mkazi wa Buguruni.
Yasin Goba, mkazi wa Kigamboni amesema ndege hizo ni fahari ya Tanzania na angependa zifanye safari kwenda Uingereza, Marekani na China.
Amesema amefurahi kuona Rais Magufuli anatekeza Ilani ya CCM ya mwaka 2015 huku akijigamba kwamba chama hicho tawala kitashinda tena kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Pia Soma
- Vikwazo kwa Zimbabwe vyazua mengine mapya
- Mwanajeshi wa Urusi awafyatulia wenzake risasi
- Rais Magufuli aagiza hospitali kujengwa wilayani Ubungo