Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wainunulia gari shule ya Serikali

C97c03c2960254e663cbdf01a1601eaa.png Wananchi wainunulia gari shule ya Serikali

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Wazazi wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya wasichana Nyankumbu inayomilikiwa na Serikali wilayani Geita mkoani hapa wamefanikiwa kununua gari ili kuleta suluhisho kwa wagonjwa shuleni hapo.

Akizungumuza wakati wa uzinduzi wa gari hilo juzi, Mkuu wa Shule hiyo Georgia Mugashe amesema gari hilo limenunuliwa takribani Sh. milioni 15 kati yake Sh. milioni 14 ikiwa ni michango ya wazazi.

Amesema wazazi wamefikia uamuzi huo baada ya kushirikishwa juu ya ukosefu wa gari la wagonjwa kwenye shule hiyo yenye wanafunzi 1012 na hivo kuamua kutoa ushirikiano.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi akizindua gari hilo amewapongeza wazazi kwa hatua hiyo kubwa na kusisitiza matumizi sahihi ya gari hilo.

“Nitoe angalizo kwa uongozi kuangalia gari hilo, litumike kwa kazi kusudiwa, lisije likatumika vinginevyo likaleta kilio kwa wazazi.

“Gari hili tumelitoa kwa shughuli A linaenda kutumika kwa shuguli B, kwa hiyo nasisitiza matumizi ya gari hili yawe yaliyipitishwa na yaliyoamuliwa,” ameeleza.

Amesema kitendo kilichofanywa na wazazi hao ni cha kuigwa kwenye maeneo mengine kwani kinalenga kuokoa maisha ya watoto hasa pale wanapokuwa wanahitaji msaada wa haraka.

Mussa Masanja mmoja ya wazazi hao amesema wametekeleza mkakati huo pasipo kushinikizwa kwa kuwa lina manufaa kwa maisha ya wanafunzi na walimu wawapo shuleni.

Stephania Masesa ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni hapo amekiri awali walikuwa wakipata changamoto ya usafiri hasa nyakati za usiku anapotokea mgonjwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz