Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi waimwagia Dawasa kero 400, yazitatua

49257 Dawasa+pic

Fri, 29 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa) imesema katika kipindi cha siku sita za maadhimisho ya wiki ya maji jijini Dar es Salaam walikusanya kero 400 kutoka kwa wananchi.

Taarifa iliyotolewa leo na Dawasa imesema katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kati ya Machi 16 hadi 20, wananchi walitoa malalamiko 400 ambapo asilimia 70 yalipatiwa majibu.

Imesema miongoni mwa malalamiko yalikuwa ni uvujaji wa maji, usomaji wa mita pamoja na wananchi wanaoishi nje ya mji kutopatiwa huduma ya maji.

Taarifa hiyo imesema katika kuhakikisha wananchi wanaishi nje ya mji wanapata maji, Dawasa  imekuwa inkitenga asilimia 35 ya mapato yake ya ndani kutekeleza miradi mikubwa na midogo ya kuwapelekea maji wananchi hao.

“Dawasa imedhamiria kuboresha zaidi utaratibu wa kupokea maoni kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwa na dawati linalohama kutoka eneo moja hadi jingine ‘Mobile customer care desk’ ili kufikia wakazi wengi na kupokea maoni mengi zaidi lengo ikiwa ni kuboresha huduma kwa wananchi tunaowahudumia,” imesema taarifa hiyo.

Imesema katika maadhimisho hayo, Dawasa ilikuwa na shughuli mbalimbali ikiwamo kufungua dawati maalum la kupokea taarifa, kero na maoni ya wananchi juu ya huduma wanazozitoa.

“Wakazi zaidi ya 400 walitembelea dawati hilo na walitoa maoni na malalamiko mbalimbali yaliyolenga kuboresha huduma za Dawasa na asilimia 70 ya malalamiko yaliyopokelewa yalitatuliwa, malalamiko mengine yaliyohitaji ufuatiliaji wa ziada yaliwasilishwa katika idara mbalimbali ndani ya mamlaka ili kushughulikiwa,” imeongeza taarifa hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz