Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wafunga Barabara kisa ajali

Wananchi Barabara Wananchi wafunga Barabara kisa ajali

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa Kata ya Bugweto Manispaa ya Shinyanga wamelazimika kufunga barabara Kuu ya Shinyanga - Mwanza kufuatia ajali iliyosababisha kifo cha Daudi Mwandu (25) na kumjeruhi Athuman Wambura (33) mkazi wa Tambukareli.

Baadhi ya wananchi wakizungumza katika eneo la tukio wamedai kuwa ajali nyingi katika eneo hilo zimekuwa zikisababishwa na madereva ambao hawaheshimu sheria za usalama barabarani na wanaendesha vyombo vyao kwa mwendo wa kasi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi baada ya kuwasili eneo la tukio amesema jeshi hilo litaendelea kuimarisha doria za usalama barabarani ili kukabiliana na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live