Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wadai hawaogi kisa uhaba wa maji

MAJI (1) Wananchi wadai hawaogi kisa uhaba wa maji

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa kijiji cha Tupendane  kata ya Ndono wilayani Uyui wanalazimika kutumia zaidi ya saa sita kusubiri kupata maji  lita 20 kila kaya  kwa siku kutokana na uhaba wa maji katika maeneo hayo ambapo wameiomba serikali kuwapelekea  mradi wa maji utakaotatua adha hiyo

Baadhi yao wanasema hulazimika kutokuoga kutokana na kukosa maji huku muda mwingi ambao ungetumika kufanya shughuli za kimaendeleo umekuwa ukitumika kushinda visimani wakingojea kuchota maji

Tumefika katika ofisi za RUWASA wilaya ya Uyui kufahamu ipi mikakati ya serikali kutatua hali hiyo lakini hawakua tayari kutoa ufafanuazi na katika utafiti wa machapisho ya serikali kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji katika

Hotuba ya waziri wa maji Juma Aweso akiwasilisha bungeni makadilio ya mapato na matumizi ya fedha za wizara ya maji kwa mwaka 2022/2023 katika ukurasa wa  202 na 203 unaonyesha kuna miradi ya maji inayo tekelezwa kwa kipindi hicho katika wilaya ya Uyui itagharibu zaidi ya bilioni 3.9 ambapo katika kata ya Ndono ni kijiji cha Ndono pekee ndio kime orodheshwa  kuwa miongoni mwa wanufaika 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live