Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wacharuka upotevu wa Sh17 milioni, sugusugu lawamani..

Pic Fedha Data Wastaafu Wananchi wacharuka upotevu wa Sh17 milioni, sugusugu lawamani..

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa kijiji cha Pumbula kata ya Songwa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wamelalamikia upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 17 kutoka kwenye mfuko wa kijiji hicho wakiwatuhumu viongozi wa jeshi la jadi maarufu kama sugusungu hukusika na upotevu wa fedha hizo.

Wametoa malalamiko hayo wakati wa mkutano wa hadhara wa kijiji hicho kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali mkoani humo.

Akitoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa fedha hizo na namna zilivyosaidia katika ujenzi na shughuli za kimaendeleo mmoja wa wanakijiji wa kijiji cha Pumbula anasema fedha hizo zilitokana na faini za makosa mbalimbali zilizosaidia katika ujenzi wa miradi ikiwemo hospitali.

"Hizo hela zilitokana na faini za makosa mbalimbali ya sheria ndogondogo tulizojiwekea kwenye kijiji hiki ambapo zimetusaidia kutekeleza miradi tofauti tofauti ikiwemo ujenzi wa hosteli, jengo la hospitali na darasa la sekondari lakini zilizobaki zikaliwa na wasimamizi ambao ni viongizi wa sungusungu", amesema Malikiti Sosoma.

Kufuatia tuhuma hizo mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka wale wote wanaokabiliwa na tuhuma hizo kulipa haraka iwezekanavyo huku kaimu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Shinyanga John Siagi akatoa kauli juu ya suala hilo.

"Watuhumiwa wote wakamatwe maana wapo baadhi ni mashahidi walioanza kurudisha fedha atakama diwani kahusika naye atajumlishwa luhakikisha hawa wananchi fedha zao zinaendelea kuwa salama na taarifa hii tutapenda mkoa tuipate mapema ili tunapoingia kwenye mkutano wa halmashauri kuu tuwenayo tayari", amesema Siagi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live