Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wachangishana, wajenga vyumba 1510 vya madarasa

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi. Wananchi wilayani Mbozi mkoani Songwe wamejenga vyumba 1,510 vya madarasa  na matundu ya vyoo 2,400 kwa gharama ya Sh3.6 bilioni katika kipindi cha miezi miwili.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi,  John Palingo amewaeleza waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 3, 2019  kwamba waliamua kuanzisha kampeni hiyo kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa 1,380 na matundu ya vyoo 2,400.

Amesema mafaniko hayo yametokana na mwitikio wa wananchi kushiriki  na kuchangia vifaa na fedha.

Palingo amesema  baada ya kukamilisha kujenga maboma hayo hatua inayofuata ni kutafuta fedha kukamilisha majengo hayo.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi, Erick Ambakisye amesema halmashauri yake imetenga Sh50 milioni kwa kumalizia ujenzi huo, kila robo mwaka watakuwa wakitenga fedha.

 

Pia Soma

Advertisement
 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz