Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wachangishana fedha kudhibiti fisi

Fisi Aua Nguruew.jpeg Fisi

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa Kata ya Tabaruka Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wamechanga Sh800,000 kwaajili ya kuliwezesha Jeshi la Jadi la Sungusungu kupambana na fisi wanaodaiwa kula mifugo na kuwadhuru.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara leo Ijumaa Julai 15, 2023 ulioitishwa na Diwani wa Tabaruka, Sospeter Busumabu, Kamanda wa Jeshi la Jadi la Sungusungu kata hiyo, Paschal Kanyashi amesema wamekubaliana kila kaya kuchangia Sh1,000.

Amesema tayari wameshaleta wawindaji ili wakabiliane na fisi hao waliogeuka kero kwa wakazi wa eneo hilo.

Kamanda huyo alilazimika kutoa taarifa hiyo baada ya mmoja wa wananchi walioudhuria mkutano huo kulalamika kuwa licha ya kuchangishwa kiasi hicho cha fedha hawaoni kazi ikifanyika.

“Fisi wamekuwa tishio kwa wananchi wa Kata ya Tabaruka idara ya Wanyamapori wanapokuja kuwawinda fisi hawaonekani  hali inayoleta sintofahamu kwa wananchi hadi tumeamua kutumia wataalamu wa jadi watusaidie,”amesema Kanyashi

Mkazi wa Kata ya Tabaruka, Simoni John amesema uwepo wa fisi kwenye kata hiyo unaleta taharuki na kuwafanya baadhi ya wananchi wanaotaka kuhamishia makazi kwenye kata yao kuhairisha wakihofia maisha yao.

Ofisa Wanyamapori daraja la II kutoka Taasisi ya Wanyamapori, Mohamed Mpoto amesema wao wamefanya doria mara kadhaa kwenye kata hiyo bila kuwapata wanyama hao na kuwaomba wananchi kufanya utafiti kubaini maeno halisi ambayo fisi wanakaa ili waweze kufika na kuwauwa.

Diwani wa kata ya Tabaruka, Sospeter Busumabu amesema ili kukabiliana na wanyama hao vijiji vyote vya kata hiyo vimekubaliana kuchangia fedha kwa ajili ya kuwawezesha sungusungu kuwasaka na kuwadhibiti wanyama hao ambao wamekuwa kero kwa wananchi.

Ameagiza fedha hizo zitumike kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo ili kuwasaka wanyama hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live